MAURICE MARANGU lyrics : "Nishike mkono/Hold my hand"
Nishike mkono, Nishike mkono baba (2)
Lalalalalala, lalalalala(2)
Kiburi kilinijaza nikaziacha njia zako
Ukajaribu kunirejesha nikapuuza mwito wako
Nikashikana na marafiki walioasi njia zako
Ujinga ukanijaza roho bila kipimo
Sasa mimi narejea kwako nipe msamaha
Nimekosa baba kwako nipe msamaha
Anasa ni mateso, ulevi ni mateso
Usherati ni mateso woooiii, niokoe
Chorus
Nahitaji uwepo kucha kutwa jana leo na kesho
Niongoze mchana usiku kucha, niweze kutabiri ya kesho
Gizani mwangazani nibaki kwa uwepo niepushe na mateso
Nakupa mkono, (Nakupa mkono)
Chorus
Submit Corrections